Latest News

Simba SC. yatinga Fainali kombe la Mapinduzi Zanzibar

By Donmory - Friday, January 10, 2014 No Comments


Klabu ya Simba imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali ya kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga URA ya Uganda mabao 2-0.
mabao ya Simba kwenye mchezo huo yamefungwa na beki Joseph Owino pamoja na 
 
kiungo Amri Kiemba 
 huku kiungo Owen Kasule wa URA akilimwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi Ramadhani Singano.
Simba sasa itacheza fainali siku ya Jumatatu Saa 10:00 Uwanja wa Amaan na timu ya KCC pia toka nchini UGANDA iliyoitoa AZAM kwa mabao 3-2.
 Kikosi cha Msimbazi leo kilikuwa:
Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’/William Lucian 'Gallas', Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haroun Chanongo, Amri Kiemba/Said Ndemla, Ramadhani Singano ‘Messi’, Amisi Tambwe/Ramadhani Chombo ‘Redondo’ na Awadh Juma/Uhuru Suleiman. 
URA; Mugabi Yassin, Samuel Ssenkoom, Alan Munamba/James Kasibante, Mussa Doca, Jonathan Mugabi, Oscar Agaba, Augustine Nsumba, Owen Kasuule, Erisa Sekisambu/Ngama Emmanuel, Feni Ali/Milos Ilic na Hashimu Sempalia.

No Comment to " Simba SC. yatinga Fainali kombe la Mapinduzi Zanzibar "