Latest News

Latest Posts

Simba SC. yatinga Fainali kombe la Mapinduzi Zanzibar

- Friday, January 10, 2014 No Comments


Klabu ya Simba imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali ya kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga URA ya Uganda mabao 2-0.
mabao ya Simba kwenye mchezo huo yamefungwa na beki Joseph Owino pamoja na 
 
kiungo Amri Kiemba 
 huku kiungo Owen Kasule wa URA akilimwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi Ramadhani Singano.
Simba sasa itacheza fainali siku ya Jumatatu Saa 10:00 Uwanja wa Amaan na timu ya KCC pia toka nchini UGANDA iliyoitoa AZAM kwa mabao 3-2.
 Kikosi cha Msimbazi leo kilikuwa:
Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’/William Lucian 'Gallas', Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haroun Chanongo, Amri Kiemba/Said Ndemla, Ramadhani Singano ‘Messi’, Amisi Tambwe/Ramadhani Chombo ‘Redondo’ na Awadh Juma/Uhuru Suleiman. 
URA; Mugabi Yassin, Samuel Ssenkoom, Alan Munamba/James Kasibante, Mussa Doca, Jonathan Mugabi, Oscar Agaba, Augustine Nsumba, Owen Kasuule, Erisa Sekisambu/Ngama Emmanuel, Feni Ali/Milos Ilic na Hashimu Sempalia.

Official Trailer la Dhoom3

- No Comments
Hii Movie ni muendelezo wa story ambayo mara ya mwisho imechezwa na Hrithik Roshan (kwenye picha hii) mwaka 2006.
Safari hii imeendelezwa na mkali wa action Aamir Khan. Kiukweli hili ni Bonge la Movie na si la kukosa limeingia Sokoni trh.25/12/2013, ikiwa ni Wiki 3 baada ya Krrish 3 kutoka.